Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
Isaya 66:7 - Swahili Revised Union Version Kabla hajawa na uchungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto wa kiume. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mji wangu mtakatifu, ni kama mama ajifunguaye bila kuona uchungu; kabla uchungu kuanza, amekwisha zaa mtoto. Biblia Habari Njema - BHND “Mji wangu mtakatifu, ni kama mama ajifunguaye bila kuona uchungu; kabla uchungu kuanza, amekwisha zaa mtoto. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mji wangu mtakatifu, ni kama mama ajifunguaye bila kuona uchungu; kabla uchungu kuanza, amekwisha zaa mtoto. Neno: Bibilia Takatifu “Kabla hajasikia uchungu, alizaa; kabla hajapata maumivu, alizaa mtoto wa kiume. Neno: Maandiko Matakatifu “Kabla hajasikia utungu, alizaa; kabla hajapata maumivu, alizaa mtoto mwanaume. BIBLIA KISWAHILI Kabla hajawa na uchungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto wa kiume. |
Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na uchungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.
Mwanamke azaapo, ana huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni.