Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
Isaya 61:11 - Swahili Revised Union Version Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo, kama vile ardhi ioteshavyo mimea, na shamba lichipushavyo mbegu zilizopandwa humo, Mwenyezi-Mungu atasababisha uadilifu na sifa kuchomoza mbele ya mataifa yote. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo, kama vile ardhi ioteshavyo mimea, na shamba lichipushavyo mbegu zilizopandwa humo, Mwenyezi-Mungu atasababisha uadilifu na sifa kuchomoza mbele ya mataifa yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo, kama vile ardhi ioteshavyo mimea, na shamba lichipushavyo mbegu zilizopandwa humo, Mwenyezi-Mungu atasababisha uadilifu na sifa kuchomoza mbele ya mataifa yote. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota, na bustani isababishavyo mbegu kuota, ndivyo Bwana Mungu Mwenyezi atafanya haki na sifa zichipuke mbele ya mataifa yote. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota, na bustani isababishavyo mbegu kuota, ndivyo bwana Mwenyezi atafanya haki na sifa zichipuke mbele ya mataifa yote. BIBLIA KISWAHILI Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote. |
Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawayewaye kama ilivyo katika milima ya Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi.
Amka, kaskazi; nawe uje, kusi; Vumeni juu ya bustani yangu, Manukato ya bustani yatokee. Mpendwa wangu na aingie bustanini mwake, Akayale matunda yake mazuri.
Siku hiyo chipukizi la BWANA litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.
Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
Mmoja ataniambia, Kwa BWANA, peke yake, iko haki na nguvu; naam, watu watamwendea yeye, na wote waliomkasirikia watatahayarika.
Dondokeni, enyi mbingu, toka juu, Mawingu na yamwage haki; Nchi na ifunuke, ili kutoa wokovu, Nayo itoe haki ikamee pamoja; Mimi, BWANA, nimeiumba.
Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.
Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;
Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Jeuri haitasikiwa tena katika nchi yako, Ukiwa na uharibifu hazitakuwa mipakani mwako; Bali utaziita kuta zako, Wokovu, Na malango yako, Sifa.
Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; Wao ni chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe, Kazi ya mikono yangu mwenyewe, Ili mimi nitukuzwe.
Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA.
wala msimwache akae kimya, mpaka atakapouimarisha Yerusalemu, na kuufanya usifike kote duniani.
Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kulielewa; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.
nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.
Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;