Isaya 49:11 - Swahili Revised Union Version Nami nitafanya milima yangu yote kuwa njia, na njia zangu zote kuu zitainuliwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Milima yote nitaifanya kuwa njia, na barabara zangu kuu nitazitengeneza. Biblia Habari Njema - BHND Milima yote nitaifanya kuwa njia, na barabara zangu kuu nitazitengeneza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Milima yote nitaifanya kuwa njia, na barabara zangu kuu nitazitengeneza. Neno: Bibilia Takatifu Nitaifanya milima yangu yote kuwa barabara, na njia kuu zangu zitainuliwa. Neno: Maandiko Matakatifu Nitaifanya milima yangu yote kuwa barabara, na njia kuu zangu zitainuliwa. BIBLIA KISWAHILI Nami nitafanya milima yangu yote kuwa njia, na njia zangu zote kuu zitainuliwa. |
Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.
Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hadi Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri.
Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.
Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu BWANA atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde.
Naye atasema, Tutieni, tutieni, Itengenezeni njia, Ondoeni kila kizuizi Katika njia ya watu wangu.
Piteni, piteni, katika malango; Itengenezeni njia ya watu; Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake; Twekeni bendera kwa ajili ya makabila ya watu.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.