Kwa kuwa ni watu wako, na urithi wako, uliowatoa katika Misri, toka katikati ya tanuri ya chuma.
Isaya 48:10 - Swahili Revised Union Version Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuri ya mateso. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi nitawajaribu lakini si kama fedha katika tanuri. Nitawajaribu katika tanuri ya taabu. Biblia Habari Njema - BHND Mimi nitawajaribu lakini si kama fedha katika tanuri. Nitawajaribu katika tanuri ya taabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi nitawajaribu lakini si kama fedha katika tanuri. Nitawajaribu katika tanuri ya taabu. Neno: Bibilia Takatifu Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha, nimekujaribu katika tanuru la mateso. Neno: Maandiko Matakatifu Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha, nimekujaribu katika tanuru ya mateso. BIBLIA KISWAHILI Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuri ya mateso. |
Kwa kuwa ni watu wako, na urithi wako, uliowatoa katika Misri, toka katikati ya tanuri ya chuma.
Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.
Niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuri ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;
Basi, kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu; maana nisipotenda hivi, nitende nini kwa ajili ya binti ya watu wangu?
Nami nitawasafisha kwa kuwatoa waasi, na hao walionikosa; nitawatoa katika nchi wanayokaa ugenini, lakini hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Bali BWANA amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuri ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo hivi leo.
ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.