Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Isaya 42:2 - Swahili Revised Union Version Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hatalia wala hatapiga kelele, wala hatapaza sauti yake barabarani. Biblia Habari Njema - BHND Hatalia wala hatapiga kelele, wala hatapaza sauti yake barabarani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hatalia wala hatapiga kelele, wala hatapaza sauti yake barabarani. Neno: Bibilia Takatifu Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataipaza sauti yake barabarani. Neno: Maandiko Matakatifu Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataiinua sauti yake barabarani. BIBLIA KISWAHILI Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. |
Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatoa hukumu kwa uaminifu.
Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;
Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.