Isaya 41:3 - Swahili Revised Union Version Awafuatia, apita salama hata kwa njia asiyoikanyaga kamwe kwa miguu yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye huwafuatia na kupita salama; huenda kasi kana kwamba hagusi chini. Biblia Habari Njema - BHND Yeye huwafuatia na kupita salama; huenda kasi kana kwamba hagusi chini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye huwafuatia na kupita salama; huenda kasi kana kwamba hagusi chini. Neno: Bibilia Takatifu Huwafuatia na kuendelea salama, katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita. Neno: Maandiko Matakatifu Huwafuatia na kuendelea salama, katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita. BIBLIA KISWAHILI Awafuatia, apita salama hata kwa njia asiyoikanyaga kamwe kwa miguu yake. |
Ni nani aliyemwinua mmoja atokaye mashariki, ambaye katika haki amemwita mguuni pake? Ampa mataifa mbele yake, na kumtawaza juu ya wafalme; awatoa wawe kama mavumbi kwa upanga wake, kama makapi yaliyopeperushwa kwa upinde wake.
Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, BWANA, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.
Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake.