Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Isaya 40:3 - Swahili Revised Union Version

Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Sauti ya mtu aliaye nyikani: “Itengenezeni njia ya Mwenyezi Mungu jangwani, yanyoosheni mapito nyikani kwa ajili ya Mungu wetu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Sauti ya mtu aliaye: “Itengenezeni jangwani njia ya bwana, nyoosheni njia kuu nyikani kwa ajili ya Mungu wetu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Isaya 40:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Mwimbieni wimbo yeye apitaye katika mawingu, Jina lake ni YAHU; Shangilieni mbele zake.


Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.


Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipoinuka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa;


Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.


Nami nitafanya milima yangu yote kuwa njia, na njia zangu zote kuu zitainuliwa.


Naye atasema, Tutieni, tutieni, Itengenezeni njia, Ondoeni kila kizuizi Katika njia ya watu wangu.


Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijia katika hekalu lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi.


Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.