Isaya 37:8 - Swahili Revised Union Version Basi yule kamanda akarudi, akamkuta mfalme wa Ashuru anapigana vita juu ya Libna; kwa maana alikuwa amesikia ya kwamba ameondoka, akaacha Lakishi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha yule mkuu wa matowashi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru alikuwa ameondoka Lakishi, aliondoka na kumkuta akishambulia mji wa Libna. Biblia Habari Njema - BHND Kisha yule mkuu wa matowashi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru alikuwa ameondoka Lakishi, aliondoka na kumkuta akishambulia mji wa Libna. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha yule mkuu wa matowashi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru alikuwa ameondoka Lakishi, aliondoka na kumkuta akishambulia mji wa Libna. Neno: Bibilia Takatifu Jemadari wa jeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi, akamkuta mfalme akipigana na Libna. Neno: Maandiko Matakatifu Jemadari wa jeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi, akamkuta mfalme akipigana na Libna. BIBLIA KISWAHILI Basi yule kamanda akarudi, akamkuta mfalme wa Ashuru anapigana vita juu ya Libna; kwa maana alikuwa amesikia ya kwamba ameondoka, akaacha Lakishi. |
Hivyo Edomu wakaasi utawala wa Yuda hata leo; wakati huo uo nao Libna wakaasi utawala wake: kwa sababu alikuwa amemwacha BWANA, Mungu wa baba zake.
Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja hapo alipoanza kumiliki; naye akamiliki miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Hamutali, binti Yeremia wa Libna.
Kisha Yoshua akapita kutoka hapo Makeda, mpaka Libna, na Israeli wote pamoja naye, nao wakapiga Libna;
Kisha wakawapa wana wa Haruni, kuhani, Hebroni pamoja na mbuga zake za malisho yake, huo mji wa kukimbilia kwa ajili ya mwuaji, na Libna pamoja na malisho yake;