Isaya 32:9 - Swahili Revised Union Version Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, isikieni sauti yangu; enyi binti za watu msiojali, tegeni masikio yenu msikie maneno yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, mnisikilize; sikilizeni ninayosema enyi mabinti mlioridhika. Biblia Habari Njema - BHND Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, mnisikilize; sikilizeni ninayosema enyi mabinti mlioridhika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, mnisikilize; sikilizeni ninayosema enyi mabinti mlioridhika. Neno: Bibilia Takatifu Enyi wanawake wenye kuridhika sana, amkeni na mnisikilize. Enyi binti mnaojisikia kuwa salama, sikieni lile ninalotaka kuwaambia! Neno: Maandiko Matakatifu Enyi wanawake wenye kuridhika sana, amkeni na mnisikilize. Enyi binti mnaojisikia kuwa salama, sikieni lile ninalotaka kuwaambia! BIBLIA KISWAHILI Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, isikieni sauti yangu; enyi binti za watu msiojali, tegeni masikio yenu msikie maneno yangu. |
BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu.
Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia.
Wale waliokula vitu vya anasa Wameachwa peke yao njiani; Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu Wakumbatia jaa.
Huu ndio mji ule wa furaha, Uliokaa salama, Uliosema moyoni mwake, Mimi niko, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulivyokuwa ukiwa, Mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomea, Na kutikisa mkono wake.
Mwanamke kati yenu aliye mwororo na laini, ambaye hangehatarisha kuweka wayo wa mguu wake nchi kwa umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa kifuani mwake, na juu ya mwanawe, na juu ya binti yake,
Kisha walipomwambia huyo Yothamu, yeye akaenda, akasimama juu ya kilele cha kilima cha Gerizimu, akapaza sauti yake, akapiga kelele, na kuwaambia, Nisikieni mimi, enyi watu wa Shekemu, ili Mungu naye apate kuwasikia ninyi.