Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na vipuli vilivyokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu.
Isaya 3:20 - Swahili Revised Union Version na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema vitambaa vya kichwani, bangili, vibwebwe, vibweta vya marashi, hirizi, Biblia Habari Njema - BHND vitambaa vya kichwani, bangili, vibwebwe, vibweta vya marashi, hirizi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza vitambaa vya kichwani, bangili, vibwebwe, vibweta vya marashi, hirizi, Neno: Bibilia Takatifu vilemba, mikufu ya vifundo vya miguu, mshipi, chupa za manukato na hirizi, Neno: Maandiko Matakatifu vilemba, mikufu ya vifundo vya miguu, mshipi, chupa za manukato na hirizi, BIBLIA KISWAHILI na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu; |
Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na vipuli vilivyokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu.
Kisha utafanya kanzu kwa ajili ya wana wa Haruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri.
Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mniletee.
na hicho kilemba cha nguo ya kitani nzuri, na zile kofia nzuri za kitani, na hizo suruali za nguo ya kitani nzuri iliyosokotwa,
Mwambie mfalme, na mama ya mfalme, Nyenyekeeni na kuketi chini; Kwa maana vilemba vyenu vimeshuka, naam, taji la utukufu wenu.
Nikatia kishaufu puani mwako, na herini masikioni mwako, na taji zuri juu ya kichwa chako.
Watakuwa na vilemba vya kitani juu ya vichwa vyao, nao watakuwa na suruali za kitani viunoni mwao; hawatajifunga kiunoni kitu kisababishacho jasho.
Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema BWANA.