Isaya 26:16 - Swahili Revised Union Version BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mwenyezi-Mungu, walipotaabika walikutafuta, walikuomba msaada ulipowaadhibu. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mwenyezi-Mungu, walipotaabika walikutafuta, walikuomba msaada ulipowaadhibu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mwenyezi-Mungu, walipotaabika walikutafuta, walikuomba msaada ulipowaadhibu. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu, walikujia katika taabu yao, wewe ulipowarudi, waliweza kuomba kwa kunong’ona tu. Neno: Maandiko Matakatifu bwana, walikujia katika taabu yao, wewe ulipowarudi, waliweza kuomba kwa kunong’ona tu. BIBLIA KISWAHILI BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao. |
Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
waliambiao gogo la mti, Wewe u baba yangu; na kuliambia jiwe, Ndiwe uliyenizaa; kwa maana wamenipa mimi visogo, wala hawakunielekezea nyuso zao; lakini wakati wa taabu watasema, Simama ukatuokoe.
Wewe ukaaye Lebanoni, Ujengaye kiota chako katika mierezi, Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana, Upatapo uchungu kama wa mwanamke azaaye.
Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa mikesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako; Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa, Mwanzo wa kila njia kuu.
Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.
Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.
Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
Wana wa Israeli wakamwambia BWANA, “Tumefanya dhambi; tufanyie yote uyaonayo kuwa ni mema; lakini tunakusihi utuokoe siku hii ya leo”.
Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA.