Isaya 2:13 - Swahili Revised Union Version Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema dhidi ya mierezi yote ya Lebanoni, ambayo ni mirefu na mizuri, dhidi ya mialoni yote nchini Bashani; Biblia Habari Njema - BHND dhidi ya mierezi yote ya Lebanoni, ambayo ni mirefu na mizuri, dhidi ya mialoni yote nchini Bashani; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza dhidi ya mierezi yote ya Lebanoni, ambayo ni mirefu na mizuri, dhidi ya mialoni yote nchini Bashani; Neno: Bibilia Takatifu kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, na mialoni yote ya Bashani, Neno: Maandiko Matakatifu kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, na mialoni yote ya Bashani, BIBLIA KISWAHILI Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani; |
Naam, misonobari inakufurahia, Na mierezi ya Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti aliyetujia.
Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani.
Umemshutumu Bwana kwa watumishi wako, kwa kuwa umesema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani ya Lebanoni; nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misonobari yake mizuri, nami nitaingia ndani ya mahali pake palipoinuka, palipo mbali sana, msitu wa shamba lake lizaalo sana.
kwa mialoni ya Bashani wamefanya makasia yako; na sitaha zako wamezifanya kwa pembe iliyotiwa kazi ya njumu katika mti wa mihugu itokayo Kitimu.
lakini nitatuma moto juu ya Yuda, nao utayateketeza majumba ya Yerusalemu. Hukumu kwa Israeli.