Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wamevikwa nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi.
Isaya 2:1 - Swahili Revised Union Version Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Neno alilopewa Isaya, mwana wa Amozi, kuhusu Yuda na Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND Neno alilopewa Isaya, mwana wa Amozi, kuhusu Yuda na Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Neno alilopewa Isaya, mwana wa Amozi, kuhusu Yuda na Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu: Neno: Maandiko Matakatifu Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu: BIBLIA KISWAHILI Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu. |
Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wamevikwa nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi.
Haya ni maono ya Isaya, mwana wa Amozi aliyoyaona kuhusu Yuda na Yerusalemu, siku za Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.
Maneno ya Amosi, aliyekuwa mmoja wa wachungaji wa Tekoa; maono aliyoyaona katika habari za Israeli, siku za Uzia, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli, miaka miwili kabla ya tetemeko la nchi.
Hili ndilo neno la BWANA lililomjia Mika, Mmoreshathi, katika siku za Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona kuhusu Samaria na Yerusalemu.
Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.
Sauti ya BWANA inaulilia mji, na mtu mwenye akili ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza.