Isaya 2:2 - Swahili Revised Union Version2 Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema2 Siku zijazo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utaimarishwa kupita milima yote, utainuliwa juu ya vilima vyote. Mataifa yote yatamiminika huko, Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND2 Siku zijazo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utaimarishwa kupita milima yote, utainuliwa juu ya vilima vyote. Mataifa yote yatamiminika huko, Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza2 Siku zijazo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utaimarishwa kupita milima yote, utainuliwa juu ya vilima vyote. Mataifa yote yatamiminika huko, Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu2 Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la Mwenyezi Mungu utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, utainuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatamiminika huko. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu2 Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la bwana utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, utainuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatamiminika huko. Tazama suraBIBLIA KISWAHILI2 Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Tazama sura |
Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi.
Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa joto; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.
Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa mamlaka ya kutoa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala kuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.