Hao samaki waliokuwa mtoni nao wakafa; na ule mto ukatoa uvundo, Wamisri wasipate kunywa maji ya mtoni; na ile damu ilikuwa katika nchi yote ya Misri.
Isaya 19:8 - Swahili Revised Union Version Na wavuvi wataugua, na wote wavuao kwa ndoana watahuzunika, nao watandao jarife juu ya maji watazimia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wavuvi watalia na kuomboleza, wote watumiao ndoana watalalama; wote wanaotanda nyavu majini watakufa moyo. Biblia Habari Njema - BHND Wavuvi watalia na kuomboleza, wote watumiao ndoana watalalama; wote wanaotanda nyavu majini watakufa moyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wavuvi watalia na kuomboleza, wote watumiao ndoana watalalama; wote wanaotanda nyavu majini watakufa moyo. Neno: Bibilia Takatifu Wavuvi watalia na kuomboleza, wote watupao ndoana katika Mto Naili, na watupao nyavu katika maji watadhoofika kwa majonzi. Neno: Maandiko Matakatifu Wavuvi watalia na kuomboleza, wale wote watupao ndoano katika Mto Naili, watadhoofika kwa majonzi. BIBLIA KISWAHILI Na wavuvi wataugua, na wote wavuao kwa ndoana watahuzunika, nao watandao jarife juu ya maji watazimia. |
Hao samaki waliokuwa mtoni nao wakafa; na ule mto ukatoa uvundo, Wamisri wasipate kunywa maji ya mtoni; na ile damu ilikuwa katika nchi yote ya Misri.
Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana.
Yeye huwatoa wote kwa ndoana yake, huwakamata katika wavu wake, na kuwakusanya katika juya lake; ndiyo sababu afurahi na kupendezwa.
Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu;