Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha BWANA; kwa hiyo BWANA akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao.
Isaya 15:9 - Swahili Revised Union Version Maana maji ya Dimoni yamejaa damu; maana ninatayarisha msiba mpya juu ya Dimoni, simba juu ya watu wa Moabu waliokimbia, na juu ya mabaki yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maji ya Diboni yamejaa damu, lakini Mungu ataongeza msiba wa Diboni. Hao wachache watakaobaki hai na kukimbia kutoka nchini Moabu, watapelekewa simba wa kuwaua. Biblia Habari Njema - BHND Maji ya Diboni yamejaa damu, lakini Mungu ataongeza msiba wa Diboni. Hao wachache watakaobaki hai na kukimbia kutoka nchini Moabu, watapelekewa simba wa kuwaua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maji ya Diboni yamejaa damu, lakini Mungu ataongeza msiba wa Diboni. Hao wachache watakaobaki hai na kukimbia kutoka nchini Moabu, watapelekewa simba wa kuwaua. Neno: Bibilia Takatifu Maji ya Dimoni yamejaa damu, lakini bado nitaleta pigo jingine juu ya Dimoni: simba juu ya wakimbizi wa Moabu na juu ya wale wanaobaki katika nchi. Neno: Maandiko Matakatifu Maji ya Dimoni yamejaa damu, lakini bado nitaleta pigo jingine juu ya Dimoni: simba juu ya wakimbizi wa Moabu na juu ya wale wanaobaki katika nchi. BIBLIA KISWAHILI Maana maji ya Dimoni yamejaa damu; maana ninatayarisha msiba mpya juu ya Dimoni, simba juu ya watu wa Moabu waliokimbia, na juu ya mabaki yao. |
Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha BWANA; kwa hiyo BWANA akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao.
Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu.
Nami nitaamrisha juu yao namna nne, asema BWANA; upanga uue, na mbwa wararue, na ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza.
Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadneza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.
Tena ikiwa baada ya hayo hamtaki kunisikiza, ndipo nitawaadhibu zaidi mara saba kwa ajili ya dhambi zenu.
ndipo nami nitawaendea kinyume katika ghadhabu yangu; nami nitawaadhibu mara saba kwa dhambi zenu.
Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
Tumewapigia mishale; Heshboni umepotea mpaka Diboni, Nasi tumeharibu mpaka Nofa, Ifikiayo Medeba.