Isaya 15:8 - Swahili Revised Union Version Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kilio kimezuka pote nchini Moabu, maombolezo yao yamefika Eglaimu, naam, yamefika mpaka Beer-elimu. Biblia Habari Njema - BHND Kilio kimezuka pote nchini Moabu, maombolezo yao yamefika Eglaimu, naam, yamefika mpaka Beer-elimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kilio kimezuka pote nchini Moabu, maombolezo yao yamefika Eglaimu, naam, yamefika mpaka Beer-elimu. Neno: Bibilia Takatifu Mwangwi wa kilio chao umefika hadi mpakani mwa Moabu, kilio chao cha huzuni kimefika hadi Eglaimu, maombolezo yao hadi Beer-Elimu. Neno: Maandiko Matakatifu Mwangwi wa kilio chao umefika hadi mpakani mwa Moabu, kilio chao cha huzuni kimefika hadi Eglaimu, maombolezo yao hadi Beer-Elimu. BIBLIA KISWAHILI Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu. |
Maana maji ya Dimoni yamejaa damu; maana ninatayarisha msiba mpya juu ya Dimoni, simba juu ya watu wa Moabu waliokimbia, na juu ya mabaki yao.
Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana.
Kutoka huko wakasafiri kwenda Beeri; ni kisima ambacho BWANA alimwambia Musa, Uwakutanishe watu, nami nitawapa maji.