Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.
Isaya 13:12 - Swahili Revised Union Version nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitawafanya watu kuwa wachache kuliko dhahabu safi; binadamu watakuwa wachache kuliko dhahabu ya Ofiri. Biblia Habari Njema - BHND Nitawafanya watu kuwa wachache kuliko dhahabu safi; binadamu watakuwa wachache kuliko dhahabu ya Ofiri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitawafanya watu kuwa wachache kuliko dhahabu safi; binadamu watakuwa wachache kuliko dhahabu ya Ofiri. Neno: Bibilia Takatifu Nitawafanya wanadamu kuwa adimu kuliko dhahabu safi, watakuwa wachache sana kuliko dhahabu ya Ofiri. Neno: Maandiko Matakatifu Nitawafanya wanadamu kuwa adimu kuliko dhahabu safi, watakuwa wachache sana kuliko dhahabu ya Ofiri. BIBLIA KISWAHILI nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. |
Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.
Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti samawi.
Binti za wafalme wamo Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki. Katika mkono wako wa kulia amesimama malkia Akiwa amevaa dhahabu safi ya Ofiri.
Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.
Na siku hiyo wanawake saba watamshika mwanaume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
Ndipo nilipouliza, Ee Bwana, hata lini? Naye akanijibu, Hadi miji itakapokuwa ukiwa, haina wenyeji, na nyumba zitakapokuwa hazina watu, na nchi hii itakapokuwa ganjo kabisa;
hadi BWANA atakapowahamisha watu waende mbali sana, na mahame yatakapokuwa mengi ndani ya nchi.