Wawezaje, basi, kurudisha nyuma uso wa ofisa mmoja wa watumishi walio wadogo wa bwana wangu, na kuitumainia Misri upewe magari na farasi?
Isaya 10:8 - Swahili Revised Union Version Maana asema, Je! Wakuu wangu si wote wafalme? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana alisema: “Je, si kweli majemadari wangu ni wafalme? Biblia Habari Njema - BHND Maana alisema: “Je, si kweli majemadari wangu ni wafalme? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana alisema: “Je, si kweli majemadari wangu ni wafalme? Neno: Bibilia Takatifu Maana asema, ‘Je, wafalme wote si majemadari wangu? Neno: Maandiko Matakatifu Maana asema, ‘Je, wafalme wote si majemadari wangu? BIBLIA KISWAHILI Maana asema, Je! Wakuu wangu si wote wafalme? |
Wawezaje, basi, kurudisha nyuma uso wa ofisa mmoja wa watumishi walio wadogo wa bwana wangu, na kuitumainia Misri upewe magari na farasi?
Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema, Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru.
Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache.
Basi sasa, tafadhali mpe bwana wangu, mfalme wa Ashuru, dhamana, nami nitakupa farasi elfu mbili, ikiwa wewe kwa upande wako waweza kupandisha watu juu yao.
BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;
Maana Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitamleta Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mfalme wa wafalme, juu ya Tiro toka kaskazini, pamoja na farasi, na magari ya vita, na wapanda farasi, na jeshi, na watu wengi.
Basi kimo chake kilitukuzwa kuliko miti yote ya shambani, na vitanzu vyake viliongezeka; matawi yake yakawa marefu, kwa sababu ya maji mengi, alipoyachipuza.
Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;
Naam, ijapokuwa waajiri kati ya mataifa, sasa nitawakusanya; nao wanaanza kupunguka kwa sababu ya mzigo wa mfalme wa wakuu.