Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria.
Hosea 10:7 - Swahili Revised Union Version Katika habari za Samaria, mfalme wake amekatiliwa mbali, kama povu usoni pa maji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme wa Samaria atachukuliwa, kama kipande cha mti juu ya maji. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme wa Samaria atachukuliwa, kama kipande cha mti juu ya maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme wa Samaria atachukuliwa, kama kipande cha mti juu ya maji. Neno: Bibilia Takatifu Samaria na mfalme wake wataelea kama kijiti juu ya maji. Neno: Maandiko Matakatifu Samaria na mfalme wake wataelea kama kijiti juu ya uso wa maji. BIBLIA KISWAHILI Katika habari za Samaria, mfalme wake amekatiliwa mbali, kama povu usoni pa maji. |
Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria.
Lakini malaika wa BWANA akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni?
Na Hoshea mwana wa Ela akamfitinia Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
Mfalme wa Ashuru akaona fitina katika huyo Hoshea; kwa maana alikuwa ametuma wajumbe kwa So, mfalme wa Misri, wala hakumletea kodi mfalme wa Ashuru, kama alivyofanya mwaka kwa mwaka; kwa hiyo mfalme wa Ashuru akamfunga, akamtia kifungoni.
Hivyo ndivyo Betheli atakavyowatenda ninyi, kwa sababu ya ubaya wenu mwingi; wakati wa mapambazuko mfalme wa Israeli atakatiliwa mbali kabisa.
Yakini sasa watasema, Hatuna mfalme; kwa maana hatumchi BWANA; na mfalme huyu je! Aweza kututendea nini?
Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.
ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.