Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe.
Hesabu 9:18 - Swahili Revised Union Version Kwa amri ya BWANA Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya BWANA walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walisafiri kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, na kupiga kambi tena kwa amri yake. Muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, watu walikaa katika kambi hiyo. Biblia Habari Njema - BHND Walisafiri kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, na kupiga kambi tena kwa amri yake. Muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, watu walikaa katika kambi hiyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walisafiri kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, na kupiga kambi tena kwa amri yake. Muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, watu walikaa katika kambi hiyo. Neno: Bibilia Takatifu Kwa amri ya Mwenyezi Mungu Waisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu lilipokaa juu ya Maskani, Waisraeli walibaki kambini. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa amri ya bwana Waisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu liliposimama juu ya Maskani, Waisraeli walibaki wamepiga kambi. BIBLIA KISWAHILI Kwa amri ya BWANA Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya BWANA walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao. |
Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe.
Hata lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, wana wa Israeli walimtii BWANA, na hawakusafiri.
Na pengine lile wingu lilikaa juu ya maskani siku chache; ndipo kwa amri ya BWANA walikaa katika kambi yao, tena kwa amri ya BWANA walisafiri.
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende kwayo.