Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.
Hesabu 9:12 - Swahili Revised Union Version wasisaze kitu chake chochote hadi asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wasibakize chakula chochote hadi asubuhi, wala wasivunje hata mfupa mmoja wa wanyama wa Pasaka. Wataiadhimisha sikukuu hii ya Pasaka kulingana na kanuni zake zote. Biblia Habari Njema - BHND Wasibakize chakula chochote hadi asubuhi, wala wasivunje hata mfupa mmoja wa wanyama wa Pasaka. Wataiadhimisha sikukuu hii ya Pasaka kulingana na kanuni zake zote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wasibakize chakula chochote hadi asubuhi, wala wasivunje hata mfupa mmoja wa wanyama wa Pasaka. Wataiadhimisha sikukuu hii ya Pasaka kulingana na kanuni zake zote. Neno: Bibilia Takatifu Wasibakize chochote hadi asubuhi wala wasivunje mifupa ya mwana-kondoo. Wanapoiadhimisha Pasaka, hawana budi kufuata masharti yote. Neno: Maandiko Matakatifu Wasibakize chochote hadi asubuhi wala wasivunje mifupa ya mwana-kondoo. Wakati wanapoadhimisha Pasaka, hawana budi kufuata masharti yote. BIBLIA KISWAHILI wasisaze kitu chake chochote hadi asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika. |
Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.
Na aliwe ndani ya nyumba moja; usiichukue nje ya nyumba nyama yake yoyote; wala msivunje mfupa wake uwao wote.
Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu.
Kwa maana lile wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.
Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, wakati wa jioni, mtaiadhimisha kwa wakati wake ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama hukumu zake zote zilivyo, ndivyo mtakavyoisherehekea.