Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 9:12 - Swahili Revised Union Version

12 wasisaze kitu chake chochote hadi asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Wasibakize chakula chochote hadi asubuhi, wala wasivunje hata mfupa mmoja wa wanyama wa Pasaka. Wataiadhimisha sikukuu hii ya Pasaka kulingana na kanuni zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Wasibakize chakula chochote hadi asubuhi, wala wasivunje hata mfupa mmoja wa wanyama wa Pasaka. Wataiadhimisha sikukuu hii ya Pasaka kulingana na kanuni zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Wasibakize chakula chochote hadi asubuhi, wala wasivunje hata mfupa mmoja wa wanyama wa Pasaka. Wataiadhimisha sikukuu hii ya Pasaka kulingana na kanuni zake zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Wasibakize chochote hadi asubuhi wala wasivunje mifupa ya mwana-kondoo. Wanapoiadhimisha Pasaka, hawana budi kufuata masharti yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Wasibakize chochote hadi asubuhi wala wasivunje mifupa ya mwana-kondoo. Wakati wanapoadhimisha Pasaka, hawana budi kufuata masharti yote.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 wasisaze kitu chake chochote hadi asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.

Tazama sura Nakili

Hesabu 9:12
7 Marejeleo ya Msalaba  

Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.

BWANA akawaambia Musa na Haruni, Amri ya Pasaka ni hii; mtu mgeni asimle;

Na aliwe ndani ya nyumba moja; usiichukue nje ya nyumba nyama yake yoyote; wala msivunje mfupa wake uwao wote.

Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu.

Kwa maana lile wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.

Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, wakati wa jioni, mtaiadhimisha kwa wakati wake ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama hukumu zake zote zilivyo, ndivyo mtakavyoisherehekea.

Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo