Basi wanangu, msiyapuuze haya, kwa kuwa BWANA amewachagua ninyi msimame mbele yake, kumhudumia, nanyi mpate kuwa watumishi wake, mkafukize uvumba.
Hesabu 8:6 - Swahili Revised Union Version Watwae Walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kisha uwatakase. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Watenge Walawi kutoka Waisraeli, uwatakase. Biblia Habari Njema - BHND “Watenge Walawi kutoka Waisraeli, uwatakase. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Watenge Walawi kutoka Waisraeli, uwatakase. Neno: Bibilia Takatifu “Watwae Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli wengine na uwatakase. Neno: Maandiko Matakatifu “Watwae Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli wengine na uwatakase kwa kawaida ya ibada. BIBLIA KISWAHILI Watwae Walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kisha uwatakase. |
Basi wanangu, msiyapuuze haya, kwa kuwa BWANA amewachagua ninyi msimame mbele yake, kumhudumia, nanyi mpate kuwa watumishi wake, mkafukize uvumba.
Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.
Kisha kuhani atakayemtakasa atamsimamisha huyo mtu atakayetakaswa, pamoja na vitu vile vyote, mbele za BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania;
naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea BWANA dhabihu katika haki.
Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu kutoka kwa uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.
Na wakati huo BWANA alilitenga kabila la Lawi ili walichukue lile sanduku la Agano la BWANA, wasimame mbele ya BWANA kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.