Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Hesabu 6:14 - Swahili Revised Union Version

naye atasongeza sadaka yake kwa BWANA, mwana-kondoo mmoja dume wa mwaka mmoja asiye na dosari, kuwa sadaka ya kuteketezwa, na mwana-kondoo jike mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari, kuwa sadaka ya dhambi, na kondoo dume mmoja asiye na dosari kwa sadaka ya amani,

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

na kumtolea Mwenyezi-Mungu zawadi zake: Mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mwanakondoo jike mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; na kondoo dume mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya amani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

na kumtolea Mwenyezi-Mungu zawadi zake: Mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mwanakondoo jike mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; na kondoo dume mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya amani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

na kumtolea Mwenyezi-Mungu zawadi zake: mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mwanakondoo jike mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; na kondoo dume mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya amani.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hapo atatoa sadaka zake kwa Mwenyezi Mungu: mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kondoo jike wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya amani,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hapo atatoa sadaka zake kwa bwana: yaani, mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kondoo mke wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya amani,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

naye atasongeza sadaka yake kwa BWANA, mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari, kuwa sadaka ya kuteketezwa, na mwana-kondoo jike mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari, kuwa sadaka ya dhambi, na kondoo dume mmoja asiye na dosari kuwa sadaka ya amani,

Tazama sura
Tafsiri zingine



Hesabu 6:14
12 Marejeleo ya Msalaba  

hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, wakachinja ng'ombe saba, na kondoo dume saba.


Kafara za vinono nitakutolea, Pamoja na fukizo la kondoo dume, Nitatoa ng'ombe pamoja na mbuzi.


Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo wawili wa kiume wasio na dosari, na mwana-kondoo mmoja wa kike wa mwaka wa kwanza asiye na dosari, na sehemu tatu za kumi za efa moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi moja ya mafuta.


Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia BWANA, kwamba ni katika kundi la kondoo; dume au jike, atamtoa huyo aliye mkamilifu.


Na mtu yeyote kati ya watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kukusudia, kwa kufanya neno lolote katika hayo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, naye akapata hatia;


Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu.


Tena kama mtu mmoja akifanya dhambi pasipo kujua, ndipo atasongeza mbuzi mmoja wa kike wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya dhambi.


bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na dosari wala waa, yaani, ya Kristo.