Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Hesabu 5:16 - Swahili Revised Union Version Basi kuhani atamleta mwanamke akaribie, na kumweka mbele za BWANA; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kuhani atampeleka huyo mwanamke karibu, na kumsimamisha mbele ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND “Kuhani atampeleka huyo mwanamke karibu, na kumsimamisha mbele ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kuhani atampeleka huyo mwanamke karibu, na kumsimamisha mbele ya Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Kuhani atamleta huyo mwanamke na kumsimamisha mbele za Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Kuhani atamleta huyo mwanamke na kumsimamisha mbele za bwana. BIBLIA KISWAHILI Basi kuhani atamleta mwanamke akaribie, na kumweka mbele za BWANA; |
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.
ndipo huyo mume atamchukua mkewe, aende naye kwa kuhani, naye ataleta sadaka yake kwa ajili yake, yaani, sehemu ya kumi ya efa; asitie mafuta juu yake, wala asitie ubani juu yake; maana, ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho ya kukumbukia uovu.
kisha kuhani atatwaa maji matakatifu katika chombo cha udongo; kisha kuhani atatwaa katika vumbi lililo pale chini ya maskani, na kulitia katika hayo maji;
Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.