Hizi ni amri, maagizo na sheria, BWANA alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.
Hesabu 4:37 - Swahili Revised Union Version Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za Wakohathi, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA kwa mkono wa Musa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hii ndiyo idadi ya watu wa jamaa ya Kohathi, ambao walihudumu katika hema la mkutano, ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Biblia Habari Njema - BHND Hii ndiyo idadi ya watu wa jamaa ya Kohathi, ambao walihudumu katika hema la mkutano, ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hii ndiyo idadi ya watu wa jamaa ya Kohathi, ambao walihudumu katika hema la mkutano, ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Neno: Bibilia Takatifu Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wote wale wa koo za Wakohathi ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Musa na Haruni waliwahesabu kufuatana na amri ya Mwenyezi Mungu kupitia kwa Musa. Neno: Maandiko Matakatifu Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wote wale wa koo za Wakohathi ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Musa na Haruni waliwahesabu kufuatana na amri ya bwana kupitia kwa Musa. BIBLIA KISWAHILI Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za Wakohathi, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA kwa mkono wa Musa. |
Hizi ni amri, maagizo na sheria, BWANA alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.
Na katika Kohathi ni jamaa ya Waamrami, na jamaa ya Waishari, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya hao Wauzieli; hizo ni jamaa za Wakohathi.
tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, kila aliyeingia kufanya kazi ya utumishi, na kazi ya kuchukua mizigo katika hema ya kukutania,
Kwa amri ya BWANA, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama BWANA alivyomwagiza Musa.