Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 26:46 - Swahili Revised Union Version

46 Hizi ni amri, maagizo na sheria, BWANA alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

46 Hayo ndiyo masharti, maagizo na sheria ambazo Mwenyezi-Mungu aliwapa watu wa Israeli kule mlimani Sinai kwa njia ya Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

46 Hayo ndiyo masharti, maagizo na sheria ambazo Mwenyezi-Mungu aliwapa watu wa Israeli kule mlimani Sinai kwa njia ya Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

46 Hayo ndiyo masharti, maagizo na sheria ambazo Mwenyezi-Mungu aliwapa watu wa Israeli kule mlimani Sinai kwa njia ya Mose.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

46 Hizi ndizo amri, sheria na pia masharti ambazo Mwenyezi Mungu alifanya kati yake mwenyewe na Waisraeli katika Mlima Sinai kupitia kwa Musa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

46 Hizi ndizo amri, sheria na pia masharti ambazo bwana alifanya kati yake mwenyewe na Waisraeli katika Mlima Sinai kupitia kwa Musa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

46 Hizi ni amri, maagizo na sheria, BWANA alizozifanya kati yake na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.

Tazama sura Nakili




Walawi 26:46
15 Marejeleo ya Msalaba  

Uliwaongoza watu wako kama kundi, Kwa mkono wa Musa na Haruni.


Kisha BWANA akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia,


Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Haya ndiyo maagizo, BWANA aliyomwagiza Musa kwa ajili ya wana wa Israeli katika mlima wa Sinai.


ambazo BWANA alimwagiza Musa katika mlima wa Sinai, siku hiyo aliyowaagiza wana wa Israeli wamtolee BWANA matoleo yao, huko katika jangwa la Sinai.


Basi Haruni na wanawe wakafanya mambo hayo yote BWANA aliyoyaagiza kwa mkono wa Musa.


Haya ndiyo maagizo na hukumu, ambayo BWANA aliwaagiza wana wa Israeli, kwa mkono wa Musa, hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.


Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za Wakohathi, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.


Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.


Hizi ndizo amri na hukumu mtakazofuataa kuzifanya katika nchi aliyokupa BWANA, Mungu wa baba zako, uimiliki, siku zote mtakazoishi juu ya nchi.


Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.


Haya ndiyo maneno ya agano BWANA alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.


Musa alituagiza torati, Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo.


Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.


Na hii ndiyo sheria, amri na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayovuka kuimiliki;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo