Basi Musa akawaambia, Kama mtafanya jambo hili; kama mtajivika silaha, ili kutangulia mbele ya BWANA mwende vitani,
Hesabu 32:21 - Swahili Revised Union Version tena kama kila mume wa kwenu mwenye kuchukua silaha atavuka Yordani mbele ya BWANA, hata atakapokuwa amekwisha watoa adui zake mbele yake, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila mpiganaji wenu atavuka mto Yordani na mkiwa chini ya uongozi wa Mwenyezi-Mungu, mtawashambulia adui zetu mpaka Mwenyezi-Mungu awashinde, Biblia Habari Njema - BHND Kila mpiganaji wenu atavuka mto Yordani na mkiwa chini ya uongozi wa Mwenyezi-Mungu, mtawashambulia adui zetu mpaka Mwenyezi-Mungu awashinde, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila mpiganaji wenu atavuka mto Yordani na mkiwa chini ya uongozi wa Mwenyezi-Mungu, mtawashambulia adui zetu mpaka Mwenyezi-Mungu awashinde, Neno: Bibilia Takatifu na kama ninyi nyote mtaenda mmejivika silaha ng’ambo ya Yordani mbele za Mwenyezi Mungu hadi awe amewafukuza adui zake mbele zake, Neno: Maandiko Matakatifu na kama ninyi nyote mtakwenda mmejivika silaha ng’ambo ya Yordani mbele za bwana mpaka awe amewafukuza adui zake mbele zake, BIBLIA KISWAHILI tena kama kila mwanamume wa kwenu mwenye kuchukua silaha atavuka Yordani mbele za BWANA, hata atakapokuwa amekwisha watoa adui zake mbele yake, |
Basi Musa akawaambia, Kama mtafanya jambo hili; kama mtajivika silaha, ili kutangulia mbele ya BWANA mwende vitani,
na hiyo nchi kushindwa mbele za BWANA; ndipo baadaye mtarudi, nanyi mtakuwa hamna hatia mbele za BWANA, wala kwa Israeli; na nchi hii itakuwa milki yenu mbele za BWANA.
Likumbukeni neno lile alilowaamuru Musa mtumishi wa BWANA, akisema, BWANA, Mungu wenu, anawapa ninyi raha, naye atawapa nchi hii.