Hesabu 28:5 - Swahili Revised Union Version pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta ya kupondwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kila mmoja atatolewa pamoja na sadaka ya nafaka ya kilo moja ya unga uliochanganywa pamoja na lita moja ya mafuta bora yaliyopondwa. Biblia Habari Njema - BHND kila mmoja atatolewa pamoja na sadaka ya nafaka ya kilo moja ya unga uliochanganywa pamoja na lita moja ya mafuta bora yaliyopondwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kila mmoja atatolewa pamoja na sadaka ya nafaka ya kilo moja ya unga uliochanganywa pamoja na lita moja ya mafuta bora yaliyopondwa. Neno: Bibilia Takatifu kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini ya mafuta ya zeituni. Neno: Maandiko Matakatifu kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini ya mafuta ya zeituni. BIBLIA KISWAHILI pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta ya kupondwa. |
Nawe utaitoa sadaka ya unga pamoja nayo kila siku asubuhi, sehemu ya sita ya efa moja, na sehemu ya tatu ya hini moja ya mafuta; kuchanganya na unga ule mzuri; sadaka ya unga kwa BWANA daima, kwa amri ya milele.
Na mtu atakapomtolea BWANA matoleo ya sadaka ya unga, matoleo yake yatakuwa ya unga mwembamba; naye ataumiminia mafuta, na kutia na ubani juu yake;
Ni sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, iliyoamriwa huko katika mlima wa Sinai iwe harufu ya kupendeza, sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa moto.
na matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha uzani wake ni shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga;