Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 2:1 - Swahili Revised Union Version

1 Na mtu atakapomtolea BWANA matoleo ya sadaka ya unga, matoleo yake yatakuwa ya unga mwembamba; naye ataumiminia mafuta, na kutia na ubani juu yake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Mtu yeyote akileta sadaka ya nafaka kwa Mwenyezi-Mungu, sadaka hiyo iwe ya unga laini. Atautia mafuta na ubani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Mtu yeyote akileta sadaka ya nafaka kwa Mwenyezi-Mungu, sadaka hiyo iwe ya unga laini. Atautia mafuta na ubani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Mtu yeyote akileta sadaka ya nafaka kwa Mwenyezi-Mungu, sadaka hiyo iwe ya unga laini. Atautia mafuta na ubani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 “ ‘Mtu yeyote aletapo sadaka ya nafaka kwa Mwenyezi Mungu, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 “ ‘Mtu yeyote aletapo sadaka ya nafaka kwa bwana, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Na mtu atakapomtolea BWANA matoleo ya sadaka ya unga, matoleo yake yatakuwa ya unga mwembamba; naye ataumiminia mafuta, na kutia na ubani juu yake;

Tazama sura Nakili




Walawi 2:1
31 Marejeleo ya Msalaba  

na mkate usiotiwa chachu, na maandazi yasiyotiwa chachu yaliyokandwa kwa mafuta, na kaki zisizotiwa chachu zilizotiwa mafuta; utazifanya za unga mzuri mwembamba wa ngano.


Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani.


Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi.


Akaniambia, Hapa ndipo mahali pa makuhani, watakapoitokosa sadaka ya hatia, na sadaka ya dhambi, watakapoioka sadaka ya unga; kusudi wasizilete nje katika ua wa nje, na kuwatakasa watu.


Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA; Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.


Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?


Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo wawili wa kiume wasio na dosari, na mwana-kondoo mmoja wa kike wa mwaka wa kwanza asiye na dosari, na sehemu tatu za kumi za efa moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi moja ya mafuta.


Nawe utatia ubani safi juu ya kila mstari, ili uwe ukumbusho kwa hiyo mikate, sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa moto.


Lakini asipowaweza hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, ndipo hapo atakapoleta matoleo yake kwa ajili ya neno hilo alilolikosa, sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, kuwa sadaka yake ya dhambi; asitie mafuta juu yake, wala ubani usitiwe juu yake; maana, ni sadaka ya dhambi.


na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, naye atasamehewa; katika jambo lolote alifanyalo hata akapata kuwa mwenye hatia kwalo.


Kisha akaisongeza sadaka ya unga, na kutwaa konzi humo, na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi.


na ng'ombe dume, na kondoo dume, kwa sadaka za amani, ili kuwachinja mbele za BWANA; na sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta; kwa maana, BWANA hivi leo atawatokea.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


Vitu hivi vitakuwa vyako katika vile vilivyo vitakatifu sana, visiteketezwe motoni; matoleo yao yote, maana, kila sadaka yao ya unga, na kila sadaka yao ya dhambi, na kila sadaka yao ya hatia watakayonitolea, vitakuwa vitakatifu sana kwa ajili yako wewe na kwa wanao.


pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta ya kupondwa.


pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri hiyo;


na matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha uzani wake ni shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga;


yeye akasongeza matoleo yake, sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa ni sadaka ya unga;


Kisha na watwae ng'ombe dume mmoja mchanga, na sadaka yake ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, nawe utatwaa ng'ombe dume mchanga mwingine kuwa sadaka ya dhambi.


Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.


Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.


Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.


Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,


Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, akiwa na chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo