Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
Hesabu 24:6 - Swahili Revised Union Version Mfano wa bonde zimetandwa, Mfano wa bustani kando ya mto, Mfano wa mishubiri aliyoipanda BWANA, Mfano wa mierezi kando ya maji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni kama mabonde yanayotiririka maji, kama bustani kandokando ya mto, kama mishubiri aliyopanda Mwenyezi-Mungu, kama mierezi kandokando ya maji. Biblia Habari Njema - BHND Ni kama mabonde yanayotiririka maji, kama bustani kandokando ya mto, kama mishubiri aliyopanda Mwenyezi-Mungu, kama mierezi kandokando ya maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni kama mabonde yanayotiririka maji, kama bustani kandokando ya mto, kama mishubiri aliyopanda Mwenyezi-Mungu, kama mierezi kandokando ya maji. Neno: Bibilia Takatifu “Kama mabonde, yanaenea, kama bustani kando ya mto, kama miti ya udi iliyopandwa na Mwenyezi Mungu, kama mierezi kando ya maji. Neno: Maandiko Matakatifu “Kama mabonde, yanaenea, kama bustani kando ya mto, kama miti ya udi iliyopandwa na bwana, kama mierezi kando ya maji. BIBLIA KISWAHILI Mfano wa bonde zimetandwa, Mfano wa bustani kando ya mto, Mfano wa mishubiri aliyoipanda BWANA, Mfano wa mierezi kando ya maji. |
Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Mavazi yako yote hunukia manemane Na udi na mdalasini. Katika majumba ya pembe Vinubi vimekufurahisha.
Nilishukia katika bustani ya milozi, Ili kuyatazama machipuko ya bondeni; Nione kama mzabibu umechanua, Kama mikomamanga imetoa maua.
Nitapanda katika jangwa mwerezi, mshita, mhadasi, na mbono; nitatia katika nyika mberoshi, mtidhari, na mteashuri pamoja;
Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.
Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa BWANA, nafaka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng'ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa.
Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayataisha kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa.
Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu.