Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
Hesabu 24:23 - Swahili Revised Union Version Akatunga mithali yake akasema, Ole wao! Ni nani atakayepona, Mungu atakapofanya haya? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena Balaamu akatoa kauli hii: “Lo! Nani ataishi, Mungu atakapofanya hayo? Biblia Habari Njema - BHND Tena Balaamu akatoa kauli hii: “Lo! Nani ataishi, Mungu atakapofanya hayo? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena Balaamu akatoa kauli hii: “Lo! Nani ataishi, Mungu atakapofanya hayo? Neno: Bibilia Takatifu Ndipo akatoa ujumbe wake: “Ole wao! Ni nani ataweza kuishi Mungu atakapofanya hili? Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo akatoa ujumbe wake: “Lo, ni nani atakayeweza kuishi wakati Mungu atakapofanya hili? BIBLIA KISWAHILI Akatunga mithali yake akasema, Ole wao! Ni nani atakayepona, Mungu atakapofanya haya? |
Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo;
Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu, Nazo zitamtaabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha, Yeye naye atapata uharibifu.