Hesabu 16:7 - Swahili Revised Union Version vitieni na moto, mkaweke na uvumba juu yake mbele za BWANA kesho; kisha itakuwa ya kwamba mtu atakayechaguliwa na BWANA, yeye atakuwa mtakatifu; inawatosha ninyi, enyi wana wa Lawi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema mweke makaa ya moto ndani na kutia ubani juu yake, kisha mtavipeleka mbele ya Mwenyezi-Mungu. Halafu tutaona ni nani aliyechaguliwa na Mwenyezi-Mungu. Nyinyi Walawi mmepita kikomo!” Biblia Habari Njema - BHND mweke makaa ya moto ndani na kutia ubani juu yake, kisha mtavipeleka mbele ya Mwenyezi-Mungu. Halafu tutaona ni nani aliyechaguliwa na Mwenyezi-Mungu. Nyinyi Walawi mmepita kikomo!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza mweke makaa ya moto ndani na kutia ubani juu yake, kisha mtavipeleka mbele ya Mwenyezi-Mungu. Halafu tutaona ni nani aliyechaguliwa na Mwenyezi-Mungu. Nyinyi Walawi mmepita kikomo!” Neno: Bibilia Takatifu kesho wekeni moto na uvumba kwenye hivyo vyetezo mbele za Mwenyezi Mungu. Mtu ambaye Mwenyezi Mungu atamchagua atakuwa ndiye mtakatifu. Ninyi Walawi mmejitukuza sana!” Neno: Maandiko Matakatifu kesho wekeni moto na uvumba kwenye hivyo vyetezo mbele za bwana. Mtu ambaye bwana atamchagua atakuwa ndiye mtakatifu. Ninyi Walawi mmejitukuza sana!” BIBLIA KISWAHILI vitieni na moto, mkaweke na uvumba juu yake mbele za BWANA kesho; kisha itakuwa ya kwamba mtu atakayechaguliwa na BWANA, yeye atakuwa mtakatifu; inawatosha ninyi, enyi wana wa Lawi. |
nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, BWANA naye yuko kati yao; ya nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa BWANA?
kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi BWANA ataonesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake.
kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;