Ndipo BWANA akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena.
Hesabu 16:25 - Swahili Revised Union Version Basi Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu; na wazee wa Israeli wakafuatana naye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Mose akaenda kwa Dathani na Abiramu, akifuatwa na wazee wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Mose akaenda kwa Dathani na Abiramu, akifuatwa na wazee wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Mose akaenda kwa Dathani na Abiramu, akifuatwa na wazee wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu, nao wazee wa Israeli wakafuatana naye. Neno: Maandiko Matakatifu Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu, nao wazee wa Israeli wakafuatana naye. BIBLIA KISWAHILI Basi Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu; na wazee wa Israeli wakafuatana naye. |
Ndipo BWANA akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena.
Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;
Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu.
Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao chochote, msiangamizwe katika dhambi zao zote.