Hesabu 15:22 - Swahili Revised Union Version Tena mtakapokosa, msiyashike maagizo hayo yote BWANA aliyomwambia Musa, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Lakini ikiwa mtakosa kuzifuata amri zote ambazo mimi Mwenyezi-Mungu nimewapa kwa njia ya Mose, Biblia Habari Njema - BHND “Lakini ikiwa mtakosa kuzifuata amri zote ambazo mimi Mwenyezi-Mungu nimewapa kwa njia ya Mose, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Lakini ikiwa mtakosa kuzifuata amri zote ambazo mimi Mwenyezi-Mungu nimewapa kwa njia ya Mose, Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Basi kama pasipo kukusudia umeshindwa kushika mojawapo katika amri hizi ambazo Mwenyezi Mungu alimpa Musa, Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Basi kama pasipo kukusudia umeshindwa kushika mojawapo katika amri hizi ambazo bwana alimpa Musa, BIBLIA KISWAHILI Tena mtakapokosa, msiyashike maagizo hayo yote BWANA aliyomwambia Musa, |
Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu yeyote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lolote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lolote la maneno hayo;
Mtawala atakapofanya dhambi, na kutenda pasipo kukusudia neno lolote kati ya hayo ambayo BWANA, Mungu wake, aliyazuilia yasifanywe, naye amepata hatia;
Na mtu yeyote kati ya watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kukusudia, kwa kufanya neno lolote katika hayo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, naye akapata hatia;
Na huyo kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake ambayo katika mambo hayo mojawapo amefanya dhambi, naye atasamehewa; na unga uliosalia utakuwa wa kuhani, kama hiyo sadaka ya unga ilivyokuwa.
hayo yote BWANA aliyowaagiza kwa mkono wa Musa, tangu siku hiyo BWANA aliyoleta maagizo, na baadaye katika vizazi vyenu
Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.