Kama idadi ilivyo ya hao mtakaowaandaa, ndivyo mtakavyofanya kwa kila mmoja, sawa na idadi yao.
Hesabu 15:13 - Swahili Revised Union Version Wote ambao wamezaliwa kwenu watafanya hayo yote kwa kufuata mfano huo, katika kusongeza sadaka kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila mwananchi Mwisraeli atafuata maagizo hayo wakati anapotoa tambiko, harufu impendezayo Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Kila mwananchi Mwisraeli atafuata maagizo hayo wakati anapotoa tambiko, harufu impendezayo Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila mwananchi Mwisraeli atafuata maagizo hayo wakati anapotoa tambiko, harufu impendezayo Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Kila mmoja ambaye ni mzawa ni lazima afanye vitu hivi kwa njia hii hapo aletapo sadaka ya kuteketezwa kwa moto kama harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Kila mmoja ambaye ni mzawa ni lazima afanye vitu hivi kwa njia hii hapo aletapo sadaka ya kuteketezwa kwa moto kama harufu nzuri inayompendeza bwana. BIBLIA KISWAHILI Wote ambao wamezaliwa kwenu watafanya hayo yote kwa kufuata mfano huo, katika kusongeza sadaka kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA. |
Kama idadi ilivyo ya hao mtakaowaandaa, ndivyo mtakavyofanya kwa kila mmoja, sawa na idadi yao.
Tena ikiwa mgeni amekaa kwenu, au mtu yeyote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye anataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa BWANA; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo hivyo.