Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 15:14 - Swahili Revised Union Version

14 Tena ikiwa mgeni amekaa kwenu, au mtu yeyote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye anataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa BWANA; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Na kama kuna mgeni anayeishi pamoja nanyi kwa muda au daima, akitaka kutoa sadaka yake kwa kuiteketeza, harufu impendezayo Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atafanya kama mnavyofanya nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Na kama kuna mgeni anayeishi pamoja nanyi kwa muda au daima, akitaka kutoa sadaka yake kwa kuiteketeza, harufu impendezayo Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atafanya kama mnavyofanya nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Na kama kuna mgeni anayeishi pamoja nanyi kwa muda au daima, akitaka kutoa sadaka yake kwa kuiteketeza, harufu impendezayo Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atafanya kama mnavyofanya nyinyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa vizazi vijavyo, wakati wowote mgeni au mtu mwingine yeyote anayeishi miongoni mwenu aletapo sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu, ni lazima afanye sawasawa kabisa na jinsi mnavyofanya ninyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa vizazi vijavyo, wakati wowote mgeni au mtu mwingine yeyote anayeishi miongoni mwenu aletapo sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kumpendeza bwana, ni lazima afanye sawasawa kabisa na jinsi mnavyofanya ninyi.

Tazama sura Nakili




Hesabu 15:14
5 Marejeleo ya Msalaba  

(maana watasikia habari za jina lako kuu, na za mkono wako ulio hodari, na za mkono wako ulionyoshwa); atakapokuja na kuomba kuielekea nyumba hii;


Nena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote, uwaambie, Mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au wa wageni walio katika Israeli, atakayetoa matoleo yake, kama ni mojawapo ya nadhiri zao, au kama ni sadaka yoyote ya hiari, watakayomtolea BWANA kuwa sadaka ya kuteketezwa;


Wala msisongeze chakula cha Mungu wenu katika wanyama hao mmojawapo kitokacho mkononi mwa mgeni; kwa sababu uharibifu wao uko ndani yao, wana kilema ndani yao; hawatakubaliwa kwa ajili yenu.


Wote ambao wamezaliwa kwenu watafanya hayo yote kwa kufuata mfano huo, katika kusongeza sadaka kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.


Katika huo mkutano, kutakuwa na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye pamoja nanyi; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kama ninyi mlivyo, na mgeni atakuwa vivyo hivyo mbele za BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo