Hagai 1:5 - Swahili Revised Union Version Basi sasa, BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa, asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Fikirini kama mnafanya sawa! Biblia Habari Njema - BHND Sasa, asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Fikirini kama mnafanya sawa! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa, asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Fikirini kama mnafanya sawa! Neno: Bibilia Takatifu Sasa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Zitafakarini vyema njia zenu. Neno: Maandiko Matakatifu Sasa hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu. BIBLIA KISWAHILI Basi sasa, BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. |
na yeye asiyelitia moyoni neno la BWANA akawaacha watumishi wake na wanyama wake mashambani.
Kwa sababu atafakari, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.
Mtu yule akaniambia, Mwanadamu, tazama kwa macho yako, sikia kwa masikio yako, ukaweke moyoni mwako, yote nitakayokuonesha; maana umeletwa hapa kusudi nikuoneshe haya; tangaza habari ya yote utakayoyaona kwa nyumba ya Israeli.
Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.
Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?
Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka.
Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kubakiza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.
Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake.