Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; sembuse Mbenyamini huyu? Mwacheni alaani, kwa sababu BWANA ndiye aliyemwagiza.
Filemoni 1:12 - Swahili Revised Union Version niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moyo wangu hasa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa namrudisha kwako, naye ni kama moyo wangu mimi mwenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Sasa namrudisha kwako, naye ni kama moyo wangu mimi mwenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa namrudisha kwako, naye ni kama moyo wangu mimi mwenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa. Neno: Maandiko Matakatifu Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa. BIBLIA KISWAHILI niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moyo wangu hasa; |
Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; sembuse Mbenyamini huyu? Mwacheni alaani, kwa sababu BWANA ndiye aliyemwagiza.
Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema BWANA.
Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [
Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa bado mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu.
tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mama yako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;
ambaye mimi nilitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako, niwapo katika kifungo kwa ajili ya Injili.