Ndipo mfalme akatuma majibu; Kwa Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng'ambo ya Mto, Salamu; na kadhalika.
Ezra 5:7 - Swahili Revised Union Version Walimtumia ripoti; na maneno haya yakaandikwa ndani yake; Kwa Dario, mfalme Salamu sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ifuatayo ni ripoti waliyompelekea mfalme: “Kwa mfalme Dario; tunakutakia amani. Biblia Habari Njema - BHND Ifuatayo ni ripoti waliyompelekea mfalme: “Kwa mfalme Dario; tunakutakia amani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ifuatayo ni ripoti waliyompelekea mfalme: “Kwa mfalme Dario; tunakutakia amani. Neno: Bibilia Takatifu Taarifa waliyompelekea ilisomeka kama ifuatavyo: Kwa Mfalme Dario: Salamu kwa moyo mkunjufu. Neno: Maandiko Matakatifu Taarifa waliyompelekea ilisomeka kama ifuatavyo: Kwa Mfalme Dario: Salamu kwa moyo mkunjufu. BIBLIA KISWAHILI Walimtumia ripoti; na maneno haya yakaandikwa ndani yake; Kwa Dario, mfalme Salamu sana. |
Ndipo mfalme akatuma majibu; Kwa Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng'ambo ya Mto, Salamu; na kadhalika.
Hii ndiyo nakala ya waraka ambao; Tatenai, Mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzake wa Kiajemi, waliokuwako huko ng'ambo ya Mto; walimtumia mfalme Dario.
Na ajue mfalme ya kuwa sisi tuliingia nchi ya Yuda, tukafika kunako nyumba ya Mungu mkuu, iliyojengwa kwa mawe makubwa, na miti imetiwa katika kuta zake, na kazi hii inaendelea kwa bidii, na kusitawi katika mikono yao.
Mfalme Nebukadneza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu.
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.