Tena walikuwako wafalme wakuu juu ya Yerusalemu, waliotawala nchi yote iliyo ng'ambo ya Mto; wakapewa kodi, na ada, na ushuru.
Ezra 4:21 - Swahili Revised Union Version Sasa toeni amri kuwakomesha watu hawa kazi yao, mji huu usijengwe, hadi nitakapotoa amri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo, toeni amri watu hao waache kuujenga upya mji huo hadi hapo nitakapotoa maagizo mengine. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo, toeni amri watu hao waache kuujenga upya mji huo hadi hapo nitakapotoa maagizo mengine. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo, toeni amri watu hao waache kuujenga upya mji huo hadi hapo nitakapotoa maagizo mengine. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo toeni amri kwa watu hawa wasimamishe ujenzi, ili mji huu usiendelee kujengwa hadi nitakapoagiza. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo toeni amri kwa watu hawa wasimamishe ujenzi, ili kwamba mji huu usiendelee kujengwa hadi nitakapoagiza. BIBLIA KISWAHILI Sasa toeni amri kuwakomesha watu hawa kazi yao, mji huu usijengwe, hadi nitakapotoa amri. |
Tena walikuwako wafalme wakuu juu ya Yerusalemu, waliotawala nchi yote iliyo ng'ambo ya Mto; wakapewa kodi, na ada, na ushuru.
Tena jihadharini, msilegee katika jambo hili; kwa nini madhara yazidi, na wafalme wapate hasara?