Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Esta 2:2 - Swahili Revised Union Version

Basi watumishi wa mfalme waliomhudumia walimwambia, Mfalme na atafutiwe mabikira vijana wazuri;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Basi, watumishi wake, waliokuwa wanamhudumia yeye binafsi, wakamshauri, “Kuna wasichana wengi wazuri; kwa nini usitafutiwe mmoja?

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Basi, watumishi wake, waliokuwa wanamhudumia yeye binafsi, wakamshauri, “Kuna wasichana wengi wazuri; kwa nini usitafutiwe mmoja?

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Basi, watumishi wake, waliokuwa wanamhudumia yeye binafsi, wakamshauri, “Kuna wasichana wengi wazuri; kwa nini usitafutiwe mmoja?

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kisha watumishi waliomhudumia mfalme walipendekeza, “Watafutwe wanawali mabikira wazuri wa sura kwa ajili ya mfalme.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kisha watumishi waliomhudumia mfalme walipendekeza, “Na ufanyike utafiti kwa ajili ya wanawali mabikira wazuri wa sura kwa ajili ya mfalme.

Tazama sura

Swahili Roehl Bible 1937

Ndipo, vijana wa mfalme waliomtumikia waliposema: Watu na wamtafutie mfalme vijana wa kike, walio wanawali wenye sura nzuri!

Tazama sura
Tafsiri zingine



Esta 2:2
6 Marejeleo ya Msalaba  

Basi ikawa Abramu alipofika Misri, Wamisri wakamwona huyo mwanamke ya kwamba yeye ni mzuri sana.


Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate joto


Katika siku ya saba, mfalme alipofurahiwa moyo wake kwa divai, aliwaamuru Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi, wale Matowashi saba, wasimamizi wa nyumba saba waliohudumu mbele zake,


na karibu naye wameketi Karshena, Shethari, Admatha, Tarshishi, Meresi, Marsena, na Memukani, wale wakuu saba wa Uajemi na Umedi, waliouona uso wa mfalme, na kuketi wa kwanza katika ufalme; akawauliza,


naye mfalme aweke wasimamizi katika mikoa yote ya ufalme wake, ili wakusanye pamoja mabikira vijana wazuri wote waende Susa, mji mkuu kwenye nyumba ya wanawake mikononi mwa Hegai, msimamizi wa nyumba ya mfalme, mwenye kuwalinda wanawake; tena wapewe vifaa vya utakaso.


Walipokuwa wangali wakisema naye, matowashi wa mfalme walifika, wakahimiza kumleta Hamani katika karamu ile aliyoiandaa Esta.