Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Esta 2:3 - Swahili Revised Union Version

3 naye mfalme aweke wasimamizi katika mikoa yote ya ufalme wake, ili wakusanye pamoja mabikira vijana wazuri wote waende Susa, mji mkuu kwenye nyumba ya wanawake mikononi mwa Hegai, msimamizi wa nyumba ya mfalme, mwenye kuwalinda wanawake; tena wapewe vifaa vya utakaso.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Unaweza kuteua maofisa katika kila mkoa wa utawala wako, na kuwaagiza wawalete wasichana wazuri wote kwenye nyumba ya wanawake hapa Susa, mji mkuu. Halafu wawekwe chini ya uangalizi wa Hegai, towashi mwangalizi wa wanawake wako; na hapo wapewe mafuta na vifaa vingine ili wajirembeshe zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Unaweza kuteua maofisa katika kila mkoa wa utawala wako, na kuwaagiza wawalete wasichana wazuri wote kwenye nyumba ya wanawake hapa Susa, mji mkuu. Halafu wawekwe chini ya uangalizi wa Hegai, towashi mwangalizi wa wanawake wako; na hapo wapewe mafuta na vifaa vingine ili wajirembeshe zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Mfalme na awateue maafisa katika kila jimbo la himaya yake kuwaleta hao wanawali wote wazuri wa sura katika nyumba ya wanawake katika ngome ya mji wa Shushani. Kisha wawekwe chini ya uangalizi wa Hegai, towashi wa mfalme, aliyekuwa msimamizi wa wanawake; na wapewe huduma zote za urembo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Mfalme na ateue maafisa katika kila jimbo la himaya yake kuwaleta hao wanawali wote wazuri wa sura katika nyumba ya wanawake katika ngome ya mji wa Shushani. Kisha wawekwe chini ya utunzaji wa Hegai, towashi wa mfalme, msimamizi wa wanawake; na wapewe matunzo yote ya urembo.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

3 Mfalme na aweke wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, wawakusanye vijana wa kike wote walio wanawali wenye sura nzuri, wawapeleke Susani jumbani mwa mfalme na kuwatia chumbani mwa wanawake mkononi mwake Hegai aliye mtumishi wa mfalme wa nyumbani wa kuwaangalia wanawake, kisha wapewe vyombo vyao vya kutengenezea uzuri.

Tazama sura Nakili

Esta 2:3
7 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mabikira walipokusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa akiketi mlangoni pa mfalme.

Naye yule msichana atakayempendeza mfalme na awe malkia badala ya Vashti. Neno hilo likampendeza mfalme, naye akafanya hivyo.

Basi palikuwa na Myahudi mmoja huko Susa, mji mkuu; jina lake Mordekai, mwana wa Yairi, mwana wa Shimei, mwana wa Kishi, wa kabila la Benyamini;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo