Danieli 8:20 - Swahili Revised Union Version Yule kondoo dume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “ ‘Yule kondoo dume uliyemwona mwenye pembe mbili, ni wafalme wa Media na Persia. Biblia Habari Njema - BHND “ ‘Yule kondoo dume uliyemwona mwenye pembe mbili, ni wafalme wa Media na Persia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “‘Yule kondoo dume uliyemwona mwenye pembe mbili, ni wafalme wa Media na Persia. Neno: Bibilia Takatifu Kondoo dume mwenye pembe mbili ambaye ulimwona anawakilisha wafalme wa Umedi na Uajemi. Neno: Maandiko Matakatifu Kondoo dume mwenye pembe mbili ambaye ulimwona anawakilisha wafalme wa Umedi na Uajemi. Swahili Roehl Bible 1937 Dume la kondoo, uliyemwona mwenye pembe mbili, ndio wafalme wa Wamedi na wa Wapersia. |
Na baada yako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.
Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Ugiriki; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.
Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo dume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.