Nami nitaleta juu ya nchi ile maneno yangu yote niliyoyanena juu yake, naam, yote yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki, aliyotabiri Yeremia juu ya mataifa haya yote.
Danieli 5:31 - Swahili Revised Union Version Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema naye mfalme Dario, Mmedi, akashika utawala akiwa na umri wa miaka sitini na miwili. Biblia Habari Njema - BHND naye mfalme Dario, Mmedi, akashika utawala akiwa na umri wa miaka sitini na miwili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza naye mfalme Dario, Mmedi, akashika utawala akiwa na umri wa miaka sitini na miwili. Neno: Bibilia Takatifu naye Dario Mmedi akanyakua ufalme akiwa na miaka sitini na mbili. Neno: Maandiko Matakatifu naye Dario Mmedi akashika ufalme akiwa na miaka sitini na miwili. Swahili Roehl Bible 1937 Ufalme wake akauchukua Mmedi Dario, naye alikuwa mwenye miaka kama 62. |
Nami nitaleta juu ya nchi ile maneno yangu yote niliyoyanena juu yake, naam, yote yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki, aliyotabiri Yeremia juu ya mataifa haya yote.
Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA.
Kwa upande wangu, katika mwaka wa kwanza wa Dario, Mmedi, mimi nilisimama ili kumsaidia na kumtia nguvu.
Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme wakuu mia moja na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;
Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo;