akiwa na magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi elfu sitini; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi.
Danieli 11:43 - Swahili Revised Union Version Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibya na Wakushi watafuata nyayo zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na vito vyote vya thamani vya nchi ya Misri. Watu wa Libia na watu wa Kushi watafuata nyayo zake. Biblia Habari Njema - BHND Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na vito vyote vya thamani vya nchi ya Misri. Watu wa Libia na watu wa Kushi watafuata nyayo zake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na vito vyote vya thamani vya nchi ya Misri. Watu wa Libia na watu wa Kushi watafuata nyayo zake. Neno: Bibilia Takatifu Atamiliki hazina za dhahabu na fedha na utajiri wote wa Misri, huku Walibia na Wakushi wakijisalimisha kwake. Neno: Maandiko Matakatifu Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na utajiri wote wa Misri, pamoja na Walibia na Wakushi kwa kujisalimisha. Swahili Roehl Bible 1937 Namo mikononi mwake mwenye nguvu vitakuwamo vilimbiko vya dhahabu na vya fedha na vyombo vyote vya Misri vipendezavyo; kwa hiyo nao Walibia na Wanubi watamfuata. |
akiwa na magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi elfu sitini; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi.
Tena hao watumishi wako wote wataniteremkia kwangu mimi, nao watanisujudia, wakisema, Toka wewe, na hawa watu wote wakufuatao; na baada ya hayo nitatoka. Basi akatoka kwa Farao na hasira kuu.
Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha; naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuharibu, na kuwaondolea mbali watu wengi.
Kushi na Misri walikuwa nguvu zake, nazo zilikuwa hazina mpaka; Puti na Walibya walikuwa wasaidizi wake.
Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye.