Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 11:44 - Swahili Revised Union Version

44 Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha; naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuharibu, na kuwaondolea mbali watu wengi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

44 Lakini habari kutoka mashariki na kaskazini zitamtisha. Naye atatoka kwa hasira kubwa ili kukatilia mbali na kuangamiza wengi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

44 Lakini habari kutoka mashariki na kaskazini zitamtisha. Naye atatoka kwa hasira kubwa ili kukatilia mbali na kuangamiza wengi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

44 Lakini habari kutoka mashariki na kaskazini zitamtisha. Naye atatoka kwa hasira kubwa ili kukatilia mbali na kuangamiza wengi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

44 Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamshtua, naye ataondoka kwa ghadhabu nyingi ili kuangamiza na kuharibu wengi kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

44 Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamshtua, naye ataondoka kwa ghadhabu nyingi ili kuangamiza na kuharibu kabisa wengi.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

44 Lakini habari zitokazo upande wa maawioni kwa jua na wa kaskazini zitamstusha; ndipo, atakapoondoka kwa makali makubwa yenye moto, aje kuangamiza na kutowesha wengi.

Tazama sura Nakili




Danieli 11:44
8 Marejeleo ya Msalaba  

Na mfalme wa kusini ataingiliwa na ghadhabu, naye atatoka na kupigana naye, yaani, na mfalme wa kaskazini; naye atapanga jeshi kubwa; na jeshi hilo litawekwa mikononi mwake.


Maana merikebu za Kitimu zitakuja kupigana naye; basi atavunjika moyo, naye atarudi na kulighadhibikia hilo agano takatifu; na kutenda kadiri apendavyo; naam, atarudi, na kuwasikiliza walioacha hilo agano takatifu.


Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibya na Wakushi watafuata nyayo zake.


Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.


Na huyo wa sita akalimimina bakuli lake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.


Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo