Hapo niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadhaa; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni;
Danieli 10:2 - Swahili Revised Union Version Katika siku zile mimi, Danieli, nilikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Wakati huo, mimi Danieli, nilikuwa nikiomboleza kwa muda wa majuma matatu. Biblia Habari Njema - BHND “Wakati huo, mimi Danieli, nilikuwa nikiomboleza kwa muda wa majuma matatu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Wakati huo, mimi Danieli, nilikuwa nikiomboleza kwa muda wa majuma matatu. Neno: Bibilia Takatifu Wakati huo, mimi Danieli nikaomboleza kwa majuma matatu. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati huo, mimi Danieli nikaomboleza kwa majuma matatu. Swahili Roehl Bible 1937 Siku zile mimi Danieli nilikuwa nikikaa matanga siku za majuma matatu. |
Hapo niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadhaa; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni;
Nitamwambia Mungu, mwamba wangu, Kwa nini umenisahau? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
Kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake;
Laiti kichwa changu kingekuwa maji, na macho yangu kuwa chemchemi ya machozi, ili nipate kulia mchana na usiku kwa ajili yao waliouawa wa binti ya watu wangu!
Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.
Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni kubwa.
Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.