Siku hiyo kinywa chako kitafumbuliwa kwake aliyeokoka, nawe utasema; hutakuwa bubu tena; ndivyo utakavyokuwa ishara kwao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Danieli 10:15 - Swahili Revised Union Version Na alipokwisha kusema nami maneno hayo, nikauelekeza uso wangu chini, nikawa bubu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Alipokuwa ananiambia maneno hayo, niliangalia chini bila kuweza kuongea. Biblia Habari Njema - BHND “Alipokuwa ananiambia maneno hayo, niliangalia chini bila kuweza kuongea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Alipokuwa ananiambia maneno hayo, niliangalia chini bila kuweza kuongea. Neno: Bibilia Takatifu Alipokuwa akiniambia haya, nilisujudu, uso wangu ukigusa chini, nikawa bubu. Neno: Maandiko Matakatifu Alipokuwa akinielezea haya, nilisujudu uso wangu ukiwa umeelekea chini, nikawa bubu. Swahili Roehl Bible 1937 Aliponiambia maneno haya, nikauelekeza uso wangu chini, maana sikuweza kusema. |
Siku hiyo kinywa chako kitafumbuliwa kwake aliyeokoka, nawe utasema; hutakuwa bubu tena; ndivyo utakavyokuwa ishara kwao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
nami nitaufanya ulimi wako ugandamane na kaakaa lako, hata utakuwa bubu, wala hutakuwa mwonyaji kwao; kwa kuwa wao ni nyumba yenye kuasi.
Basi mkono wa Bwana umekuwa juu yangu wakati wa jioni, kabla hajafika yeye aliyetoroka; naye alikuwa amenifumbua kinywa changu, hata aliponijia wakati wa asubuhi; na kinywa changu kilikuwa wazi, wala sikuwa bubu tena.
Lakini niliisikia sauti ya maneno yake; nami niliposikia sauti ya maneno yake, ndipo nikashikwa na usingizi mzito, na uso wangu umeielekea nchi.
Basi alipokuwa akisema nami, nilishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.
Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake.